Rais Dkt.Samia azindua Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini

MTWARA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa, Dkt. Samia Suluhu Hassan mapema Septemba 15, 2023 amezindua Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini iliyopo Mtwara.

Rais Samia amesema kuwa kukamilika kwa Hospitali hiyo ambayo ina watalaam, vifaa na vifaatiba vya kisasa itasaidia watu wa Kanda ya Kusini inayojumuisha Mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma kupata uhakika wa huduma za matibabu ya kibingwa karibu na maeneo yao.

“Wagonjwa wote wenye matatizo makubwa watakuja hapa, jengo hili litumike kutoa huduma za afya,” amesema Rais Samia.

Rais Samia amesema kuwa kazi ya watumishi wa afya ni kuokoa maisha ya watu hivyo watumishi hao wajitumie kufanya kazi kwa kuwa Serikali imewekeza kwenye miundombinu, vifaa na dawa na wao watimize wajibu wao.
"Tunahitaji matunzo ya jengo hili, vifaa na huduma kwa wananchi kwa lugha nzuri, kila mtu amepangiwa jukumu lake na Mwenyezi Mungu, tumridhishe Mungu kwa huduma tunazozitoa, nawatakia kila la kheri,” amesema Rais Samia huku akiongezea kuwa changamoto zilizopo za watumishi zitaendelea kufanyiwa kazi kwa haraka.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news