Mheshimiwa Simbachawene akagua miradi ya TASAF


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akitoka kukagua mradi wa ujenzi wa jengo la utawala la Shule ya Sekondari Inyala Halmashauri ya Wilaya ya Geita lililofadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Mkoa wa Geita.
Sehemu ya wananchi na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Kijiji cha Inyala Kata ya Nyamigota, Halmashauri ya Wilaya ya Geita wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene wakati akizungumza na wananchi na walengwa hao wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Mkoa wa Geita.
Mwonekano wa mradi wa ujenzi wa jengo la utawala la Shule ya Sekondari Inyala Halmashauri ya Wilaya ya Geita Mkoa wa Geita lililofadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
Mlengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa Kijiji cha Inyala, Kata ya Nyamigota Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Bi. Merciana Njashi akitoa ushuhuda wa namna alivyonufaika na Mpango huo kwa Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Mkoa wa Geita.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news