Taifa Stars yafuzu Fainali AFCON 2024

ANNABA-Taifa Stars ambayo ni timu ya Taifa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekata tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

Mafanikio hayo yanakuja baada ya sare ya bila kufungana na wenyeji, Algeria katika mchezo wa mwisho wa Kundi F uliopigwa usiku wa Septemba 7, 2023 katika Dimba la Mei 19, 1956 mjini Annaba.

Taifa Stars kwa matokeo hayo inamaliza na alama nane, nyuma ya Algeria wenye alama 16 na wote wanafuzu AFCON ya Ivory Coast 2024 waking'ara mbele ya Uganda iliyomaliza na alama saba na Niger alama mbili.

Wakati huo huo, mechi nyingine ya mwisho ya Kundi F, Niger wamechapwa mabao 2-0 na Uganda Uwanja wa Marrakech nchini Morocco. 
 
Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan ameipongeza Raifa Stars kwa mafanikio hayo. 
 
"Hongereni vijana wetu wa Taifa Stars kwa kufuzu michuano ya kuwania kushiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (2023 Africa Cup of Nations). 
 
Mmeandika historia kwani hii ni mara yetu ya 3 kufuzu tangu kuanzishwa kwa mashindano haya. Nawatakia kila la kheri."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news