Waziri wa Fedha awasilisha Muswada wa Sheria ya Ununuzi wa Umma 2023 bungeni

NA PETER HAULE
WF

WAZIRI wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amewasilisha muswada wa Sheria ya Ununuzi wa Umma wa mwaka 2023 wenye dhumuni la kufangamanisha masuala ya ununuzi na ugavi katika mnyororo wa usimamizi wa ugavi.
Akiwasilisha muswada huo Septemba 7,2023 bungeni jijini Dodoma Dkt. Nchemba, alisema kuwa muswada huo utaimarisha mazingira ya ununuzi na ugavi kwa taasisi na mashirika ya umma yanayojiendesha kibiashara na kupunguza muda katika hatua na michakato ya zabuni.

“Sehemu ya muswada huu unaainisha kuendelea kuwepo kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma, malengo na majukumu yake pia imeainisha nguvu ya kisheria Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma kufanya uchunguzi, kupata taarifa, kutoa mapendekezo kwa Mlipaji Mkuu wa Serikali au Afisa Masuuli wa Taasisi ya umma inayohusika na uchunguzi,”alieleza Dkt.Nchemba.

Dkt. Nchemba alisema kuwa Mamlaka hiyo itawasilisha matokeo ya uchunguzi kwa mtu au watu wenye mamlaka ya kuchukua hatua za kinidhamu au hatua nyingine stahiki dhidi ya afisa au mtumishi na kuwasilisha taarifa maalumu kwa Waziri

Aidha imeainisha majukumu ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma ikiwemo kuomba taarifa, nyaraka na kumbukumbu ya aina yoyote, kuhusu mchakato wa ununuzi na ugavi, kutoa wito, kufanya uchunguzi na kuanzisha ukaguzi kwenye shughuli zinazohusiana na ununuzi na ugavi.

Pia, muswada huo umeainisha Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma kupendekeza kwenye chombo chenye mamlaka kuhusu kusitisha utoaji wa fedha au kuzitaka taasisi kurejesha fedha zilizopotea,

Kubadilishwa kwa Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi, kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa Afisa Masuuli, Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi, Mjumbe wa kamati ya tathmini au afisa mwingine yoyote anayehusika katika mchakato wa ununuzi na uhamisho wa muda wa majukumu ya ununuzi ya taasisi kwenda taasisi nyingine au Wakala.

Vilevile vyanzo vya mapato ya Mamlaka ambavyo vitajumuisha fedha zitakazotengwa na Bunge, mikopo au misaada, mapato yatokanayo na bidhaa au huduma zinazotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma na fedha nyingine zozote zitakazopokelewa na Mamlaka kwa kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu yake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news