TANAPA yathibitisha kuibuka kwa moto Mlima Kilimanjaro

KILIMANJARO-Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limeutangazia umma kuwa mnamo Septemba 3, 2023 moto ulizuka katika Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro, eneo la Indonet-Rongai Wilaya ya Rombo.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Septemba 8, 2023 na Catherine Mbena ambaye ni Afisa Uhifadhi Mwandamizi Kitengo cha Mawasiliano-TANAPA.

"Jumla ya wazimaji 134 walipelekwa eneo la tukio mlimani wakiwemo askari na maafisa wa Jeshi la Uhifadhi (JU), Jeshi la Akiba na wananchi wa vijiji vya jirani na mpaka sasa moto umedhibitiwa kwa asilimia kubwa.

"Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana na uchunguzi unaendelea kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama. Aidha, shughuli za utalii katika Mlima Kilimanjaro zinaendelea kama kawaida. Vikosi vingine zaidi vinaendelea kupelekwa kuhakikisha tunaudhibiti moto huu,"imefafanua sehemu ya taarifa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news