Waziri Simbachawene asisitiza mambo muhimu kwa watumishi nchini

NA RAINER BUDODI

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene, amewasisitiza watumishi wa umma nchini kuongeza elimu na ujuzi kwenye maeneo yanayohusiana na taaluma zao ili kuepusha malalamiko kati yao na waajiri.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Mkoa wa Geita katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa halmashauri hiyo.

Mhe. Simbachawene ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato mkoani Geita wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinawazokabili watumishi hao katika utekelezaji wa majukumu yao.

Amesema baadhi ya watumishi wamekuwa wakiruhusiwa na waajiri kwenda masomoni kuongeza ujuzi katika taaluma zao, lakini wakifika huko wanabadilisha na kusoma masuala mengine ambayo hayaendani na taaluma hizo na anaporudi katika kituo cha kazi anataka kubadilishiwa kada wakati mwajiri hana uhitaji huo, hivyo kusababisha malalamiko kati ya mwajiri na mtumishi.
Sehemu ya watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Mkoa wa Geita wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa halmashauri hiyo.

“Wewe ni Mwalimu umepewa ruhusa na mwajiri wako kwenda kuongeza elimu na ujuzi kwenye taaluma yako, unafika chuoni unabadilisha unasoma kitu kingine bila makubaliano na mwajiri wako na unaporudi katika kituo chako cha kazi unataka kubadilishiwa kada, hiyo ni kusababisha matatizo na mwajiri wako,” Mhe. Simbachawene amesema.

Ameongeza kuwa mtumishi anaweza kubadilishiwa kada, endapo mwajiri ataona kuna uhitaji wa kada hiyo katika eneo lake na itampasa mtumishi huyo kuanzia daraja la mwanzo kulingana na kada husika vinginevyo awe ameruhusiwa na mwajiri ambapo ataombewa mshahara binafsi,” Mhe. Simbachawene amesisitiza.
Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania, Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Mwalimu Oscar Magori akiwasilisha hoja kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha Waziri huyo na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Mkoa wa Geita kilicholenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa Mkoa huo.

Amesema Serikali ingeruhusu kila mtumishi kujiendeleza anavyotaka tofauti na kada yake ingekuwa vurugu, hivyo kuepuka vurugu hizo kila mmoja ajiendeleze kwenye taaluma yake kwa kuzingatia taratibu na miongozo ya utumishi wa umma iliyopo.

Mhe. Simbachawene anaendelea na ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani Geita yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma mkoani humo na kusikiliza changamoto za kiutumishi zinazowakabili ili kuzitatua.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news