Wizara ya Ardhi kutoa elimu nyepesi kuhusu umiliki ardhi

NA MUNIR SHEMWETA
WANMM BAGAMOYO

WAZIRI wa ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa amesema wizara yake iko mbioni kutoa elimu nyepesi kwa wananchi kuhusu hatua mbalimbali za umiliki ardhi na jinsi ardhi inavyoweza kuhamishwa kutoka mmiliki moja kwenda kwa mwingine. 
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa akizindua Kliniki ya Ardhi kwa Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani tarehe 23 Septemba 2023. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenga na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Halima Okash.

Amesema hayo Septemba 23, 2023 wakati wa akizindua Kliniki ya Ardhi kwa Wilaya ya Bagamoyo inayoendelea eneo la Mapinga mkoani Pwani.

Kwa mujibu wa Silaa, pamoja na wizara yake kuwa na jukumu la kuisimamia ardhi ipo haja kutoa elimu nyepesi kwa watanzania kwenye eneo la ardhi kuanzia inapotwaliwa, kupangwa, kupimwa na kumilikishwa hususani inapohama kutoka mmiliki mmoja kwenda mwingine. 
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kliniki ya Ardhi kwa Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani tarehe 23 Septemba 2023. Kulia ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Pauline Gekul na wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenga na kushoto Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Halima Okashi. 

"Tukitoa hiyo elimu inaweza kusaidia maana hapa kuna watu wamenunua eneo kwa mwenyekiti wa mtaa wakiamini wana eneo, lakini sheria ya ardhi haielekezi kupata eneo kwa mwenyekiti wa mtaa,"alisema.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa akisikiliza kero za wananchi wakati akizindua Kliniki ya Ardhi kwa Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani tarehe 23 Septemba 2023.  

Akifafanua zaidi, Waziri wa Ardhi amesema, anayenunua ardhi kwa mtu anao wajibu wa kujua ama kufahamu aliyemuuzia ameipataje ardhi ambapo amesema maeneo mengine na mauzo hayo yanashuhudiwa na viongozi wakiwemo wenyeviti wa vitongoji.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa akisikiliza kero za wananchi wakati akizindua Kliniki ya Ardhi kwa Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani tarehe 23 Septemba 2023. 

Hata hivyo, ameweka wazi kuwa, pamoja na wamiliki wa ardhi wa kulinda maeneo yao wanayomiliki lakini wizara yake haitaacha maeneo kama Mapinga Bagamoyo kuwa kichaka cha mtu yeyote mwenye uwezo kufanya anachotaka anafanya.

‘’Niweke wazi mimi katika uongozi wangu wizara ya ardhi nitakachofanya ni kuhakikisha nasimamia haki na siku zote haki haina rangi jinsia, haina hali ya mtu na haki ni haki,’’alisema. 
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa akipata maelezo kutoka kwa meneja wa tawi la Benki ya CRDB Bagamoyo Mkoa wa Pwani wakati wa uzinduzi Kliniki ya Ardhi kwa Wilaya ya Bagamoyo tarehe 23 Septemba 2023.

Amewataka wananchi kuheshimu sheria zinazotungwa na Bunge sambamba na kujifunza kusimamia haki zao. 

‘’Wapo baadhi ya viongozi wa wanaotumia mamlaka yao ya kutambua maeneo na kuwekea ushahidi lakini sheria ya ardhi haiwataji kama wanapaswa kufanya miamala ya ardhi,’’alisema Waziri Silaa. 
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa akitoa hati kwa mmoja wa wananchi wakati wa uzinduzi wa Kliniki ya Ardhi kwa Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani tarehe 23 Septemba 2023. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge.

‘’Tunataka na wenzetu katika majiji makubwa kama Mwanza, Dodoma Arusha, Dar, Mbeya na Pwani ambayo kiasi kikubwa inaungana na Dar es Salaam ifike wakati tufanye kazi za ardhi kwa mujibu wa sheria,"alisema. 

Awali Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Halima Okashi alieleza kuwa, Kliniki ya Ardhi waliyoianzisaha itakuwa na jukumu la kusikiliza kero za wananchi katika masuala mbalimbali ya ardhi huku akibainisha kuwa, itaendelea katika kata zote za Wilaya ya Bagamoyo. 
Sehemu ya wananchi wa Mapinga Bagamayo wakiwa katika Kliniki ya Ardhi kwa Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani tarehe 23 Septemba 2023. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI).

Uzinduzi wa Kliniki ya Ardhi katika Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani unafuatia uzinduzi wa kliniki kama hizo kwenye Wilaya ya Kigamboni na Temeke ambapo lengo kubwa ni kusikiliza na kuzitafutia ufumbuzi changamoto za sekta ya ardhi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news