Dkt.Athumani:Simiyu, MSD hawajawahi kutuchelewesha hata mara moja

SIMIYU-Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan imeendelea na maboresho ya huduma na kuhakikisha vifaa tiba vya kisasa vinafika kwa wakati kupitia Bohari ya Dawa nchini (MSD) ili kuondoa rufaa za huduma za kibingwa kwa wajawazito na watoto mkoani Simiyu.

Mratibu wa Huduma za Tiba katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Simiyu, Dkt.Seleman Athumani amesema, tayari wamepokea vifaa kutoka Bohari ya Dawa nchini (MSD).

"Vifaa ambavyo tumevipokelea leo ni vitanda ambavyo ni standard electrical ICU beds, kwa sababu katika jengo hili pia tutakuwa na huduma ya ICU kwa wale akina mama ambao wanasubiri kujifungua na tayari wamejifungua.

"Ni vitanda lakini, vitanda kwa ajili ya upasuaji, vifaa kwa ajili ya kumzalisha mama, vitanda kwa ajili ya kujifungulia,.

"Mizigo hii yote tayari ipo, MSD wameshawasilisha na vipo stoo, kwa hiyo muda wowote tutaanza kuvifunga katika maeneo ya kutolea huduma.

"Huduma za namna hii walikuwa wanapata za kujifungua tu katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mji wa Bariadi, lakini huduma za ICU kwa upande wa akina mama hazikuwepo.

"Kwa hiyo ndiyo tunakwenda kuzianzisha katika hospitali yetu ambayo ni Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu ili sasa ile adha walikuwa wanaipata ya kupelekwa Bugando tuachane nayo.

"Wananchi wote wa Mkoa wa Simiyu hususani kina mama na watoto, Mheshimiwa Rais ameshaamua kwamba wapate huduma katika maeneo yao ambayo ni bora na sisi tumejipanga kuhakikisha huduma hiyo bora inawafikia wananchi kwa haraka zaidi.

"Kwa hiyo, tupo katika hatua za mwisho za kufunga vifaa katika maeneo yetu ya kazi ili kusudi sasa wananchi waweze kuanza kupata huduma hiyo hapa hapa Simiyu.

"Kimsingi MSD hapa Simiyu tukisema tunawalaumu tutakuwa hatujawatendea haki, kwa sababu vifaa vyote tangu vimekuja ni mwaka 2022.

"MSD hawajawahi kutuchelewesha hata mara moja, hata vitanda hivi tulipowapa tu taarifa kwamba tunaanza kufanya- instalation ya vitanda vimefika hata usafi hatujafanya.

"Kwa hiyo tunawashukuru sana kwa kuzingatia, lakini vile vile kwa kujali kwamba wananchi sasa wanahitaji kupata huduma na hawatuchelewishi katika hilo."

Mratibu wa Huduma za Afya hospitalini hapo amesema kuwa, "Tunashukuru sana,kwa kuweza kupata msaada huu ambao ninajua umeletwa kutokana na juhudi za Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan.

"Ambaye wakati wote amekuwa anatoa mchango mkubwa sana katika kuboresha huduma za afya na tumepokea vitanda hivi ambavyo tutaviweka kwenye vyumba vya uangalizi maalumu kwa ajili ya mama wajawazito ambao wamejifungua au hawajajifungua.

"Kwa hiyo, ni mchango mkubwa na hii inatupa sasa nguvu ya kuhakikisha kwamba ndani ya mwezi mmoja tunaweza tukawa katika nafasi ya kuanza kutoa huduma."

Naye Daktari Bingwa wa Afya ya Uzazi na Magonjwa ya Mama, Dkt.Fredrick Mlekwa amesema, "Itoshe kusema tu kwamba, hata vipimo vya juu kama ST-Scan, hospitali hii sasa ina ST-Scan, lakini isitoshe kusema tu hayo kwamba tuna upande wa maabara, vipimo vya juu vya mambo ya uzazi na watoto wachanga vinapatikana.

"Tunafanya cation sensitivity kwenye hospitali, tunapima Hormonal Assay ambapo vipimo vyote miaka ya nyuma tulikuwa tunapeleka Bugando, sasa hivi vipimo vyote vinapatikana hapa na wataalamu tupo."

Naye Afisa Ugavi wa Usafirishaji kutoka MSD, Haruni Kikwanda amesema, amefarijika kuona kuwa, hospitali hiyo imepokea vifaa hivyo kwa furaha.

"Na wakati wanapokea vifaa hivyo, wananchi nao walikuwepo na waliipongeza Serikali yao ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan pamoja na Mkurugenzi wa MSD kwa kuwaletea vifaa hivyo kwa ajili ya matumizi ya hospitali yao."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news