SADC PF kufanya mikutano ya kupokea maoni ya wadau

DODOMA-Katibu wa Bunge anautaarifu umma kwamba Kamati za Kudumu za Jukwaa la Mabunge ya Jumuiya ya Kusini mwa Afrika (SADC PF) zitafanya Mikutano ya kupokea maoni ya wadau kwenye dhima ya ‘Amplifying Citizens’ voices in Regional Integration in Southern Africa: Bridging the Engagement Gap by Bringing Parliament to the People’.

Mikutano hiyo itafanyika tarehe 11 -18 Oktoba, 2023 kuanzia saa 5:00 asubuhi hadi saa 10:30 jioni na itafanyika kwa njia ya mtandao.

Hivyo Katibu wa Bunge anachukua fursa hii kuwaalika wadau wote ikiwemo Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kushiriki Mikutano hiyo. Kwa mawasiliano ya jinsi ya kushiriki wasiliana na Ndugu Ida Kombe kwa namba +255714360790.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news