Fahamu kwa nini Mheshimiwa Philipo Mulugo amejigaraza kwenye vumbi

NA GODFREY NNKO

ALIYEKUWA Naibu Waziri wa Elimu ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Jimbo la Songwe mkoani Songwe, Mheshimiwa Philipo Mulugo amepiga magoti kisha kujigaragaza chini kwenye vumbi ili achafuke kama walivyochafuka wananchi.

Hiyo ikiwa ni ishara ya kuwashukuru wananchi waliompokea katika ziara yake Kata ya Udinde wilayani Songwe Mkoa wa Songwe huku akitoa shilingi milioni 10 kwa ajili ya kuviwezesha vikundi 16 vya wajasiriamali katika kata hiyo.

“Thamani ya muda, thamani ya vumbi mliyopigwa leo, thamani ya jua, thamani ya vitenge kuviweka chini, havilingani hata na milioni 100,havilingani, mkaacha muda wenu wote...mitaa mbalimbali, mkakusanyika, mkasema eti mnamsubiri Philipo Mlugo aje tumpokee, tumuone tu.

"Hii thamani kubwa ya muda mliyopoteza, thamani ya vumbi, thamani ya kuweka vitenge chini, jambo hilo siwezi kulisahau katika akili yangu mpaka kifo changu,asanteni sana.

"Asante Mungu kwa kuniumba nilivyo, asante sana wana Udinde, asanteni sana, asanteni sana wana Udinde na mimi natamani nichafuke kama mlivyochafuka ninyi, nimefurahi sana, asanteni sanaa saanaa. Hata wanangu wataangalia.

"Naomba mpokee fedha kiasi cha shilingi milioni 10, kazi ya mikono yangu na jasho langu la familia yangu. Milioni 10 siyo ya mfuko wa jimbo wala siyo hela ya Serikali,ni hela ya mikono ya kazi yangu, nitatoa kwenye miradi yangu, nitazileta Udinde, vikundi vyote 16 mgawane."

Mheshimiwa Mulugo yupo katika ziara ya kibunge ya kutembelea na kukagua miradi, kuzungumza na wananchi wa jimbo hilo na viongozi wa Serikali na chama.

Hata hivyo, akiwa katika kata hiyo, amechangia shilingi milioni tatu kwa ajili ya kununua mashine ya kudurufu katika Shule ya Sekondari ya Serikali ya Philipo Mulugo iliyopo Kata ya Udinde.

Pia, mbali na kuchangia shilingi milioni 10 kwa ajili ya vikundi 16 vya ujasiriamali ametoa shilingi milioni saba za ujenzi wa soko katika Mtaa wa Nyerere uliopo Kata ya Udinde jimboni humo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news