Shirika la Masoko ya Kariakoo lafunguka kuhusu madai ya upangishaji

DAR ES SALAAM-Shirika la Masoko ya Kariakoo linaufahamisha umma na wafanyabiashara kuwa mradi wa ujenzi na ukarabati wa Soko la Kariakoo bado unaendelea na hakuna eneo la biashara lililopangishwa kwa mfanyabiashara yeyote hadi sasa.

Kwa taarifa hii, Shirika linakanusha taarifa zisizo rasmi zinazosambaa kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuwa tayari Soko la Kariakoo limeanza kupangisha maeneo ya biashara.

Taarifa rasmi kuhusu upangishaji wa maeneo yote ya biashara katika Soko la Kariakoo zitatolewa na Uongozi wa Shirika baada ya mradi kukamilika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news