Mwenyekiti wa CCM Arusha, Kamishna mstaafu Zelote Stephen afariki

DAR ES SALAAM-Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha,Kamishna mstaafu Zelote Stephen amefariki dunia jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Katibu wa CCM Mkoa Arusha, Mussa Matoroka amesema wamepata taarifa za kifo hicho jioni ya Oktoba 26,2023.

"Ni kweli Mwenyekiti amefariki jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa amekwenda kupatiwa matibabu...huu ni msiba mkubwa kwetu CCM, familia ndugu na jamii," amesema Matoroka.

Katika ukurasa wake wa Instagram, Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo ameweka picha ya marehemu Stephen huku akiandika maneno yanayoonyesha kuumizwa na kifo hicho.

“Taarifa za kuondokewa na Zelote Stephen, Mwenyekiti wetu wa CCM mkoa wa Arusha ni taarifa za kusikitisha sana. Kwani kwa hakika kifo chake kimetunyima fursa muhimu ya kuendelea kujifunza mengi na kuuishi uongozi wake"

“Mungu ameendelea kutufunza. Mipango yetu imekwama. Nenda Laigwanan. Nenda mzee wangu. Nilipokutembelea siku chache zilizopita hospitali ulinipa matumaini. Kumbe mipango ya Mungu ikabaki. Wewe ni shujaa, Nenda Kamanda,"imesomeka sehemu ya taarifa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news