Watanzania wawili hawajulikani walipo nchini Israel

DODOMA-Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inazo taarifa za kupotea kwa Watanzania wawili nchini Israel ambao ni miongoni mwa vijana 260 waliopo nchini humo kwa mafunzo ya kilimo cha kisasa.

Serikali kwa kushirikiana na Mamlaka mbalimbali nchini Israel inaendelea na juhudi za kuwapata vijana hao ili kuwaleta katika mazingira salama.

Familia za vijana hao zimejulishwa kuhusu jitihada hizo na Serikali inaendelea kuwasiliana
nao.

Watanzania tisa wanaoishi nchini Israel waliitikia wito wa mpango wa Serikali wa kuwarejesha nyumbani na walipokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, tarehe 18 Oktoba 2023.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news