Waziri Mavunde atoa onyo kali kwa mabroka nchini

DODOMA-Waziri wa Madini,Anthony Mavunde amesema atawafutia leseni mabroka wote watakaokiuka taratibu zilizowekwa na serikali pamoja na watakaojihusisha na utoroshaji wa madini.

Ameyasema hayo Oktoba 19,2023 jijini Dodoma katika kikao cha pamoja na Chama cha Mabroka wa Madini Tanzania (CHAMMATA).

Mheshimiwa Mavunde amesema,Serikali inawatambua mabroka wote kwa mujibu wa sheria ndio maana wanapewa leseni na anatamani kuwaona mabroka wananufaika kwani ni watu muhimu katika mnyororo wa biashara ya madini.

“Iwapo itathibitika mnashirikiana na dealers kutorosha madini hapo mtaacha kuwa marafiki zangu na hivi sasa tukimkamata mtu mmoja nafuatilia mnyororo mzima sitamuachi mtu hata mmoja.

"Madini yakitoroshwa Serikali ikipoteza mapato tutashindwa kujenga barabara, tutashindwa kununua madawati, tutashindwa kununua madawa hivyo mtu yeyote anaye ipenda na kuijali nchi yake atalipa uzito jambo hili.

"Msikubali kuwa ngazi ya kuwakosesha madawa, kuwakosesha barabara nzuri, kuwakosesha madawati watanzania hivyo nataka ukikaa peke yako ujitathmini,”amesema Waziri Mavunde.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mabroka wa Madini Tanzania, Jeremia Kituyo amesema, chama hicho kilianziwa 2022 jijini Dodoma.

Amesema,hadi hivi sasa wana mabadiliko ya kuwa na wanachama mabroka wenye leseni na wasio na leseni 18,638 nchi nzima licha ya kuhamasisha mabroka wote wapate leseni ili kufikia malengo ya Wizara ya Madini na wafanye biashara kihalali nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news