Nabii Mkuu Dkt.GeorDavie aishukuru Serikali kwa kumpa barabara

ARUSHA-Nabii Mkuu Mhe Dkt.GeorDavie ameishukuru serikali kwa kutambua mchango wake katika jamii na kumpa heshima ya kuandika jina lake na huduma yake kwenye barabara mbili hapa jijini Arusha ambapo kuna barabara ya GeorDavie Road na Ngurumo ya Upako Road.

Amesema kuwa, ataendelea kusaidia wananchi na kwamba furaha yake ni kusaidia watu huku akisema amefanya mambo mengi mema kwa watu na hakutarajia siku moja atapewa heshima kubwa kama hii ya kupewa Barabara ambazo zitakuwa ni historia hata kwa vizazi vijavyo.

Aidha, kwa hapa nchini hatujaona barabara nyingine yenye jina la Mtumishi wa Mungu na Nabii Mkuu Mhe Dkt.GeorDavie amekuwa Mtumishi wa Mungu wa kwanza kupewa barabara zenye jina na huduma yake ambapo GeorDavie Road ipo barabara ya kuelekea Ikulu ya Nabii Mkuu.

Kuna Barabara nyingine kama Nyerere, Ally Hassan Mwinyi, Kawawa Road, Sokoine Road na Sasa tuna Barabara ya GeorDavie na Ngurumo ya Upako Road ambapo zinapatikana Barabara ya Dodoma Arusha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

1 Comments

  1. Ongera sana mtumishi wa mungu kwa kazi mzuri mimi naitwa afande mjungaji Gibson kutoka Kenya semu ya bungoma

    ReplyDelete
Previous Post Next Post

International news