Miaka 20 jela kwa kukutwa na viungo vya sokwe mtu

KIGOMA-Mkulima na mkazi wa Kijiji cha Buhingu, Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma,Jeremiah Ngendabanka amehukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani kwa kupatikana na viungo mbalimbali vya sokwe mtu.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mahakama ya Wilaya ya Uvinza, Misana Majura Mwendesha Mashitaka Mkaguzi wa Polisi, Ephraim Mwakanyamale aliiambia mahakama kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Septemba 22, 2022.

Mwakanyamale aliieleza mahakama hiyo kuwa mshitakiwa alipatikana na nyara hizo za serikali, ambazo ni mkono mmoja wa sokwe mtu, kichwa kimoja cha sokwe mtu na ngozi moja ya sokwe mtu vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 12.

Akitoa hukumu hiyo wiki hii, Hakimu Majura amesema kuwa Mahakama imejiriridhisha pasipo shaka na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka na kumtia hatiani mtuhumiwa kwa kosa hilo.

Amesema, ametoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa wahalifu wanaojihusisha na vitendo vya uwindaji haramu

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news