Serikali yaahidi mema zaidi kupitia Uchumi wa Buluu

ZANZIBAR-Imeelezwa kwamba ufugaji wa nyuki unaweza kuunganishwa na buluu kaboni katika hifadhi ya mikoko na katika ufugaji wa viumbe maji katika maeneo mbalimbali katika kuelekea maendeleo endelevu.

Katibu Mkuu Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar, Dkt. Aboud Suleimani Jumbe, akizungumza na Ujumbe wa (IFAD) pamoja na timu ya Uratibu wa Programu ya AFDP Ofisini Kwake Mjini Unguja.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar, Dkt. Aboud Suleimani Jumbe wakati akizungumza na Ujumbe wa Shirika la Maendeleo ya Kilimo Duniani (IFAD) pamoja na timu ya Uratibu wa Programu ya AFDP Ofisini kwake Mjini Unguja.

“Kufungamanisha maeneo jumuishi yenye miradi tofauti ya uchumi Utasaidia kupata mwamko mkubwa wakujikita katika shughuli za kiuchumi,” amebainisha.
Ziara hii ya Ujumbe wa Shirika la Maendeleo ya Kilimo Duniani (IFAD) pamoja na timu ya Uratibu wa Programu ya AFDP imeonesha namna ambavyo serikali inaweza kushirikiana na sekta binafsi ili kuhakikisha dhamira ya Miradi ya Maendeleo inafanikiwa.

Aidha upo umuhimu wa kuendelea kuwawezesha wajasiriamali wetu na wakulima wetu wa mwani, wavuvi wadogo wadogo lakini pia haja ya kukabiliana na taka ngumu na maji taka katika bahari.

“Programu ya AFDP ni sehemu kubwa ya ajenda yetu ya maendeleo ya Uchumi buluu na ni ajenda ambayo viongozi wetu wa taifa wamekuwa wakifuatilia kwa karibu sana; ili kuhakikisha malengo yake yanafikiwa kwa wakati” amesema.

Bw. Richard Abila (katikati) akiongea jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar, Dkt. Aboud Suleimani wakati ujumbe huo Ulipotembelea Ofisini kwake baada ya ziara ya kutembelea miradi ya Maendeleo inayofadhiliwa na shirika hilo la maendeleo kwa kushirikiana na serikali.

Awali Mratibu wa Programu ya kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) Kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Bw, Salimu Mwinjaka amesema, ziara ya kutembelea Programu ya kuendeleza kilimo na uvuvi inayotekelezwa na IFAD na serikali imekuwa ya mafanikio sana.

Katibu Mkuu Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar, Dkt. Aboud Suleimani Jumbe akizungumza na Ujumbe wa Shirika la Maendeleo ya Kilimo Duniani (IFAD) pamoja na timu ya Uratibu wa Programu ya AFDP Ofisini kwake baada ya Kumaliza utembeleaji wa Miradi ya Maendeleo inayofadhiliwa na shirika hilo kwa Visiwa vya Pemba na Unguja.

“Tumetembelea maeneo ya uzalishaji wa Mwani tumeona mafanikio halikadhalika, Programu ya kuendeleza kilimo na Uvuvi inaangalia jinsi unavyoweza kutatua changamoto zitakazojitokeza,” alisema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news