TBA kuwachukulia hatua kali wadaiwa sugu

DAR ES SALAAM-Wakala wa Majengo Tanzania (TBA,) umesema kuwa hadi sasa jumla ya fedha kiasi cha shilingi bilioni 7.8 zinadaiwa kwa wapangaji wake zikiwemo taasisi za umma zinazotumia nyumba na majengo yake.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mtendaji Mkuu wa TBA, Arch. Daud Kondoro amesema kuwa wapangaji wote zikiwemo taasisi za umma zinatakiwa kuhakikisha zinalipa madeni yao kwa wakati kabla hatua kali hazijachukuliwa dhidi yao.

"Kwa sasa TBA imeazimia kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wapangaji wote tunaowadai, moja ya hatua zitakazochukuliwa ni kuwaondoa wadaiwa sugu kwa nguvu kwa kutumia dalali wa Mahakama ambaye amepewa zabuni hiyo kufanya kazi kwa niaba ya TBA.

"Mpaka sasa tayari dalali wa mahakama ambaye ni Twins Auction Mart amekabidhiwa orodha ya wadaiwa wote kwa hatua zinazofuata na zoezi hili litafanyika kuanzia Desemba 1, 2023 katika Mikoa yote nchini,"ameeleza Kondoro.

Aidha amesema, hatua hiyo itakwenda sambamba na kuwafungulia mashtaka wadai wote watakaoondolewa katika nyumba na majengo hayo ili kuhakikisha kuwa fedha yote inayodaiwa inakusanywa.

Vile vile ameeleza juu ya maboresho yaliyofanyika kwenye mfumo wa kielekroniki. “Kuanzia tarehe 1 Desemba, 2023, tutaanza kutumia mfumo mpya wa Kielektroniki wa Usimamizi wa Miliki za Serikali (GRMS) toleo la 2.

Mfumo huu mpya utakuwa unatoza riba ya 20% kwa mpangaji atakae kaa zaidi ya miezi 3 bila kulipa kodi ya pango. Riba hiyo itaendelea kutozwa kila mwezi kwa kiwango mfuto (automatically) cha 20% mpaka deni lote litakapokamilika kulipwa,” amesema Arch. Kondoro.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news