Waziri Silaa:Pimeni ardhi na kufuatilia hati, faida ni nyingi

KIGOMA-Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa amewataka wananchi kote nchini ambao zoezi la urasimishaji ardhi linaendelea katika maeneo yao kuhakikisha wanalipia, wanapimiwa na baadae kufuatilia hati zao ili ardhi wanayomiliki iweze kupanda thamani.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendekeo ya Makazi, Jerry Silaa akikabidhi hati kwa Bi.Furaha Kapipi Bukulu mkazi wa Kijiji cha Msimba Kata ya Mungunya kilichopo nje Kidogo ya Manispaa ya Kigoma wakati wa zoezi la ugawaji hati kwa wanachi walioshiriki zoezi la urasimishaji unaoendelea mkoani Kigoma.

Waziri Silaa alisema, utoaji huduma kwa njia ya kliniki unarahisisha kazi kwa wananchi kwani unawaondolea usumbufu, lakini pia unafanyika hadharani na mwananchi akifika anapatiwa huduma zote kesho yake anakuja kuchukua hati yake.

Waziri Silaa alisema hayo alipofika katika Kijiji cha Msimba Kata ya Mungunya kilichopo nje Kidogo ya Manispaa ya Kigoma kwa lengo la kugawa hati kwa wakazi hao ambao tayari wamekamilisha taratibu za urasimishaji.

Aidha,Waziri Silaa alitoa maelekezo kwa Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoani Kigoma kuhakikisha anafanya kazi hiyo kama ilivyo kwa maeneo mengine ili mwananchi akifika katika eneo hilo apatiwe hati yake nakuondoka.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendekeo ya Makazi, Jerry Silaa akiongea na wananchi wa Kijiji cha Msimba Kata ya Mungunya kilichopo nje Kidogo ya Manispaa ya Kigoma wakati wa zoezi la ugawaji hati kwa wanachi walioshiriki zoezi la urasimishaji unaoendelea mkoani Kigoma.

"Ninyi wenyewe mnaona kuwa si kila mwananchi anaweza kuingia katika ofisi za serikali mwingine akiingia ndani ya eneo la serikali haimwingii akilini kwani kuna wakati anaona anaonewa anaona kuna vyumba vingi vinamchanganya,’’amesema Waziri Silaa.

Waziri Silaa aliwataja watendaji kuwa waadilifu na kubainisha pia kuwa baadhi yao sio waadilifu hivyo kutajia wananchi viwango vya malipo ambavyo uchangia wananchi hao kushindwa kufuatilia huduma ya sekta ya ardhi na kuiongeza kuwa Serikali ya Rais Samia imepunguza gaharama za kulipia hati kwa 50%.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Bw.Salum Kalli amewambia wananchi waliofika katika kliniki hiyo kutambua kuwa kumilki ardhi yenye hati kuna thamani kubwa kiuchumi tofauti na wale wanaomilki ardhi bila kuirasimisha.

Watalaamu wa Sekta ya Ardhi kutoka Manispaa ya Kigoma wakiendelea na zoezi la utoaji hati kwa Wananchi wa Kijiji cha Msimba Kata ya Mungunya kilichopo nje Kidogo ya Manispaa ya Kigoma wakati wa zoezi la ugawaji hati kwa wanachi walioshiriki zoezi la urasimishaji unaoendelea Mkoani Kigoma.

Kiongozi huyo wa Wilaya alisema kuwa na hati ndiyo maisha kwani ukishakuwa na hati wewe ni tajiri kwa kuwa unakopeshaka na ukiwa na hati miliki unalinga na kubeza.

‘’Hati ni pesa, hati ni nyumba, hati ni maendeleo, hati ni Maisha ukienda Benki kama hutaki kuonga unamwonesha Meneja unasema unaona hii hati niliyonayo tayari unakuwa na pesa yenye thamani ya milioni 30,’’amesema kiongozi huyo wa wilaya.

Mkuu huyo wa Wilaya aliongeza kuwa unaweza ukawa na ardhi ndogo yenye hati ikawa na thamani kubwa kuliko ya mtu anayemiliki mashamaba makubwa ambayo hayana hati kwani anayemiliki ardhi bila kuirasimisha hawezi kutumia ardhi hiyo kama dhamana ya kujipatia mkopo benki.

Wananchi wa Kijiji cha Msimba Kata ya Mungunya kilichopo nje Kidogo ya Manispaa ya Kigoma wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ardhi, Jerry Silaa mara baada kupata hati zao wakati wa zoezi la ugawaji hati kwa wanachi walioshiriki zoezi la urasimishaji unaoendelea mkoani Kigoma.

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa muda sasa imekuwa ikiendesha zoezi Urasimishaji kote Nchini kupitia Kliniki za Ardhi kila Mkoa kwa lengo la kurasimisha ardhi na makazi lakini pia kutumia fursa hiyo kutatua Migogoro ya Ardhi kwa wananchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news