Rais wa Romania awasili rasmi Tanzania

DAR ES SALAAM-Rais wa Romania, Mheshimiwa Klaus Iohannis, amewasili nchini kwa ziara ya Kitaifa kuanzia leo tarehe 16 hadi 19 Novemba 2023 kufuatia mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere amepokelewa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angellah Kairuki (Mb.)

Lengo la ziara hiyo ni pamoja na kushawishi uwekezaji zaidi na kuvutia watalii wengi kutoka nchini Romania.
Aidha katika mazungumzo rasmi yatakayofanyika tarehe 17 Novemba 2023 Rais huyo na mwenyeji wake watajadili namna bora ya kukuza na kuimarisha ushirikiano kati sekta za elimu, afya, kilimo nishati na madini.

Kabla ya kuondoka nchini tarehe 19 Novemba 2023 Rais wa Romania atapata fursa ya kwenda Zanzibar ambapo atazungumza na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi na kutembelea mji mkongwe ambao ni moja kati ya vivutio vikubwa vya utalii duniani

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news