Bora nibariki jiwe ukajengee nyumba na sio kubariki ndoa za jinsia moja-Askofu Kassala

GEITA-Askofu wa Jimbo Katoliki Geita, Flavian Kassala amesema hayuko tayari kubariki ndoa zilizo kinyume na maadili, kwani ni kinyume na maagano ya Mungu ya kutaka binadamu wakazaliane na kuendeleza vizazi ulimwenguni.
Baba Askofu Kassala amesema,bora abariki jiwe ukajengee nyumba na sio kubariki mambo yaliyo kinyume na maadili

Akihubiri katika Misa ya Kitaifa ya Krisimasi amesema, ndoa zisizo na maadili ni kwenda kinyume na maandiko ya Mungu yanayotaka wanadamu wakazaliane na kuendeleza vizazi.

Pia, amesema binadamu anakataa uumbaji wa Mungu na kufanya mambo yaliyokatazwa huku wakitaka na kanisa liyabariki jambo ambalo amelipinga vikali

"Binadamu amemuacha Mungu na kufanya mambo yaliyokatazwa.

"Binadamu amekataa uumbaji na kuendeleza uumbaji na sasa wanafanya mambo machafu yasiyompendeza Mungu, wamekuwa wakiharibu vizazi kwa kutoa mimba na sasa wanataka tubariki ndoa zisizo na maadili, kwangu bora nibariki jiwe,lakini sio uchafu huo."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news