Naibu Waziri Pinda alivyojumuika na wananchi Sikukuu ya Krismasi jimboni

NA MUNIR SHEMWETA
WANMM

NAIBU Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amesheherekea Siku Kuu ya Krismasi akiwa katika jimbo lake la Kavuu lililopo wilaya ya Mlele mkoani Katavi.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kavuu wilayani Mlele Mkoa wa Katavi Mhe Geophrey Pinda akizungumza na baadhi ya wananchi waliomtembelea nyumbani kwake Kibaoni katika jimbo la Kavuu tarehe 25 Disemba 2023 mkoani Katavi.

Akiwa jimboni humo, Naibu Waziri Pinda alishiriki ibada ya Krismasi katika Kanisa Katoliki Parokia Teule ya Bikira Malia Mpalizwa Mbinguni Kibaoni ambako alishiriki pia harambee ya ya ujenzi wa Nyumba za Mapadri wa Kanisa hilo na kuahidi kuchangia mifuko 200 ya Saruji. ujenzi wa nyumba hizo utagharimu shilingi milioni 75.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kavuu wilayani Mlele mkoa wa Katavi Mhe Geophrey Pinda (kushoto) akimsikiliza Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mlele, Wolfgun Pinda (Katikati) akiwa jimboni kwake tarehe 25 Disemba 2023 mkoani Katavi.

Ibada hiyo ya Krismasi katika kanisa hilo ilihudhuriwa pia na Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Kayanza Peter Pinda.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kavuu wilayani Mlele mkoa wa Katavi Mhe Geophrey Pinda (katikati) akizungumza na mmoja wa wananchi wa Kibaoni, Mlele wakati akiwa jimboni kwake tarehe 25 Disemba 2023 mkoani Katavi. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mlele Wolfgun Pinda.

Aidha,Naibu Waziri Pinda akiwa eneo la Kibaoni ambapo ndipo yalipo makazi yake wilayani Mlele mkoani Katavi alijumuika na baadhi ya wananchi wa eneo hilo wakiwemo viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mlele katika kusheherekea siku hiyo ya Noeli.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kavuu wilayani Mlele mkoa wa Katavi Mhe Geophrey Pinda akisalimiana na mmoja wa wananchi waliofika nyumbani kwake Kibaoni, Mlele akiwa jimboni kwake tarehe 25 Disemba 2023 mkoani Katavi.

Naibu Waziri Pinda yuko jimboni kwake katika jimbo la Kavuu wilayani Mlele Mkoa wa Katavi pamoja na mambo mengine kujumuika na wapiga kura wake kutafakari utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika jimbo hilo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news