MAAFA KATESH:Simba SC yakabidhi msaada

DAR ES SALAAM-Klabu ya Simba imekabidhi msaada kwa ajili ya waathirika wa mafuriko na maporomoko huko Hanang' mkoani Manyara.
Akipokea misaada hiyo,Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Damas Ndumbaro aliishukuru klabu ya Simba kwa kutoa msaada huo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Simba,Salum Abdallah alisema, "Kwa niaba ya Rais wa heshima Mohammed Dewji, bodi, uongozi, wapenzi na wanachama wa Simba tunapenda kutoa pole nyingi kwa wahanga wa mafuriko na maporomoko huko Hanang'.

"Wengi wa wahanga hawa ni wapenzi wa soka, na sisi kama klabu tunaungana nao kwenye kipindi hiki kigumu".

Tukio hilo lilihudhuriwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Imani Kajula na Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo (BMT), Neema Msika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news