Rais Dkt.Samia avunja Bodi ya TANESCO, afanya uteuzi

DAR ES SALAAM-Kufuatia Balozi Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kuteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uganda tarehe 18 Desemba, 2023, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameivunja bodi hiyo.

Aidha, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Simuli.

Dkt.Nyansaho ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Benki ya Azania. Uteuzi huu unaanza mara moja.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Desemba 19,2023 na Zuhura Yunus ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news