Simba SC yaitundika mabao 2-0 Wydad Casablanca, yafufua matumaini Afrika

DAR ES SALAAM-Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam imerejesha matumaini ya kutinga hatua ya Robo Fainali ya Michuano ya Klabu Bingwa barani Afrika.

Ni baada ya kuichapa mabao 2-0 Wydad Casablanca kupitia mchezo wa kundi B uliopigwa Desemba 19,2023 katika Dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam.

Mchezo huo ulianza kwa kasi ya kawaida huku timu zikisomana, lakini Wydad walifanya mashambulizi makali mawili dakika ya 28 na 32 ingawa mlinda mlango Ayoub Lakred alikuwa imara na kuondoa hatari zote.

Willy Onana awapatia waajiri wake bao la kwanza dakika ya 35 kwa shuti kali nje kidogo ya 18 baada ya kumalizia pasi ya kifua iliyopigwa na Kibu Denis.

Dakika mbili baadae Onana naye aliwapatia bao la pili waajiri wake baada ya kumalizia pasi safi kutoka kwa Mzamiru Yassin.

Matokeo haya yameifanya Simba SC kufikisha alama tano wakipanda hadi nafasi ya pili wakiwa nyuma kwa alama mbili dhidi ya vinara ASEC Mimosas.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news