Simba SC yakabidhiwa shilingi milioni 10 kutoka kwa Rais Dkt.Samia

DAR ES SALAAM- Naibu Waziri wa Sanaa Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ amemkabidhi nahodha msaidizi wa Klabu ya Simba, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ shilingi milioni 10.

Hiyo ni sehemu ya ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa akitoa fedha taslimu kwa wawakilishi wa Tanzania kupitia michuani ya Kimataifa kupitia Kampeni ya ‘Bao la Mama’.

Rais Samia hutoa Shilingi milioni tano kwa kila bao litakalofungwa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ili kuongeza morali kwa wachezaji.

Bao la mama limeongeza morali kwa wachezaji kujituma kuisaidia timu kupata matokeo ya ushindi.

Katika mchezo wa Simba SC dhidi ya Wydad Casablanca mabao yote mawili waliyoshinda yalifungwa na kiungo mshambuliaji, Willy Onana.

Ni kupitia mtanange ambao umepigwa Desemba 19, 2023 katika Dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news