VIDEO:Mvua zasababisha vilio,maafa makubwa Katesh

NA DIRAMAKINI

WANANCHI wa Katesh katika Halmashauri ya Wilaya ya Hanang' mkoani Manyara wanahitaji misaada ya dharura baada ya makazi yao kugeuka visiwa huku mali na mifugo ikizolewa kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.

Kwa nyakati tofauti wananchi hao kutoka maeneo ya Jorodom, Ganana, Gendabi, Kwa Kimaro na kwingineko wameieleza DIRAMAKINI kuwa, unahitajika msaada wa haraka ili kuweza kuwaokoa wananchi walionasa katika matope.

Huko Gendabi wananchi wanasema, hali hiyo inafanana na Volcano ya huko nyuma ambapo maporomoko ni makubwa.

"Hapa mawe, miamba, miti mikubwa na tope yamezoa nyumba nyingi. Tumeshindwa kufika kwani hali si shwari hapaendeki. Hata Katesh Gedan’gonyi nyumba zingine zimefukiwa na tope miti na mawe.Watu wanajitahidi kutoa miti kuokoa maisha ya familia hiyo."
DIRAMAKINI inaendelea kufuatilia kwa kina tukio hili na kadri taarifa rasmi zitakavyokuwa zinapatikana zitakuwa zinakujia moja kwa moja hapa. TAZAMA VIDEO CHINI;
Idadi ya vifo vilivyotokana na janga la mafuriko hayo na majeruhi inatajwa kuwa ni makumi ya watu.

Mafuriko hayo yamesababisha uharibifu mkubwa ikiwemo baadhi ya nyumba na mali, kusombwa na maji ambapo serikali imeandaa maeneo matatu kwa ajili ya kuwapatia huduma wahanga wa mafuriko.

Shule ya Msingi Kateshi, Hanang na Dumanang zitatumika katika kuhifadhi wahanga hao na kuwataka kuhama katika maeneo yao mara moja bila kusubiri majanga wengine yatokee.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Gendabi wilaya ya Hanang, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga amesema kuwa, juhudi za serikali ni pamoja na kutuma helikopta ya jeshi ili iweze kusaidia watu walioko juu ya nyumba na miti.

Zoezi la uokoaji na kusafisha barabara linaendelea kutokana na matope yaliyofurika katika maeneo ya makazi ya watu, maeneo ya biashara na stendi ya mabasi

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news