EWURA yatangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta leo Januari 3,2024

DAR ES SALAAM-Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini zinazotumika kuanzia Jumatano, tarehe 3 Januari 2024 saa 6:01 usiku.
Kupungua kwa bei za mafuta kwa mwezi Januari 2024 ni kwa sababu ya kushuka kwa bei za mafuta (FOB) katika soko la dunia kwa wastani wa asilimia 6.03 kwa petroli na asilimia 7.13 kwa dizeli.

Pia kupungua kwa bei za mafuta kumetokana na kushuka kwa gharama za uagizaji wa mafuta kwa wastani wa asilimia 3.72 kwa petroli na asilimia 17.52 kwa dizeli kwa Bandari ya Dar es Salaam na kwa wastani wa asilimia 22.71 kwa petroli na asilimia 22.12 kwa dizeli kwa Bandari ya Mtwara. Bei za mafuta za rejareja kwa kila mji, wilaya na mkoa ni kama zinavyooneshwa katika Jedwali Na.3.

Wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa rejareja wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei zinazooneshwa katika Jedwali Na. 3.

Aidha, wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa jumla wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei zinazooneshwa katika Jedwali Na. 2. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mfanyabiashara yoyote atakayekiuka AGIZO hili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news