Apigwa 'Tanganyika jerk' mbele ya Rais Dkt.Ruto

NA DIRAMAKINI 

RAIS wa Jamhuri ya Kenya, Mheshimiwa Dkt.William Ruto ametofautiana na maafisa usalama wake siku ya Jumapili,baada ya maafisa hao kumshughulikia mwanaume aliyetatiza hotuba yake.
Mkuu wa Nchi alikuwa kwenye jukwaa huko Kakamega akihitimisha hotuba yake wakati kijana huyo ambaye hakutambulika alipokaribia, mkono wake wa kulia ukiinuliwa hewani huku akiwa ameshikilia nembo ya Serikali ya Kenya. 

Mara moja, maafisa watano walimkimbia na kumwinua mtu huyo kutoka chini, na kumpeleka mbali na jukwaa.

Kutokana na jinsi maafisa wa usalama walivyomnyanyua kwa nguvu, viatu vilivyovaliwa na kijana huyo vilitoka huku akipinga. 

Mheshimiwa Rais aliwaagiza wanausalama wasimshughulikie bali wamsindikize hadi kwenye hema la watu mashuhuri ambako angefanya naye mazungumzo mara baada ya kuhitimisha hotuba yake.

"Haya, wacha aketi hapa. Wewe mlete hapa. Leta yeye hapa. Mlete hapa aketi nitamuongelesha baadaye. Asante sana," Rais aliwaeleza wananausalama hao. (Kenyans)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news