DCEA,Polisi waendelea kuelimisha jamii kuhusu tatizo la dawa za kulevya

DODOMA-Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imesema inashiriki katika maonesho ya Wiki ya Sheria jijini Dodoma kwa lengo la kutoa elimu kwa jamii kuhusu tatizo la dawa za kulevya.
Hayo yamesemwa na Kamishna Jenerali wa mamlaka hiyo, Aretas Lyimo wakati akizumgumza na vyombo vya habari jijini Dodoma.
Amesema, maonesho hayo ni fursa muhimu kwao katika kuelimisha jamii kuhusu makosa ya dawa za kulevya na adhabu zilizoainishwa kwenye sheria ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya.
"Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya namba 5 ya mwaka 2015 inatoa adhabu kali kwa makosa mbalimbali yanayohusiana na dawa za kulevya, ikiwa ni pamoja na Kumiliki dawa za kulevya, kusafirisha dawa za kulevya, kuzalisha, kutumia n.k adhabu zake zinafikia hadi kifungo cha maisha jela."

Amesema,lengo ni kuzuia na kupambana na tatizo la dawa za kulevya kwani matumizi ya dawa za kulevya yanasababisha madhara makubwa kwa jamii, ikiwa ni pamoja na uhalifu, umaskini, magonjwa mbalimbali, uharibifu wa mazingira , uratibu, kuvunjika kwa familia n.k.
"Hivyo, natoa wito kwa wananchi wa jiji la Dodoma kutembelea banda letu ili kujifunza zaidi kuhusu dawa za kulevya, sheria zinazosimamia dawa za kulevya, na jinsi ya kujilinda dhidi ya dawa za kulevya,"amesema Kamishna Jenerali Lyimo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news