Kocha Abdelhak Benchikha awapongeza wachezaji Simba SC

ABIDJAN-Kocha Mkuu wa Simba SC,Abdelhak Benchikha amewapongeza wachezaji kwa kucheza soka safi licha ya kupata sare ugenini dhidi ya ASEC Mimosas katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Benchikha amesema, ameridhishwa na jinsi timu ilivyocheza kwa umoja na kushirikiana na kusababisha kupatikana kwa pointi moja muhimu ugenini.

Aidha,Benchikha ameongeza kuwa,kwa sasa hakuna muda wa kupumzika maandalizi ya mchezo wao wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi ya Jwaneng Galaxy ambao utapigwa mwishoni wa Juma lijalo yanaanza.

“Tunaushukuru Mungu kwa kutuwezesha kupata pointi moja ugenini, kama nilivyosema awali isingekuwa mechi rahisi, lakini tumepambana hadi mwisho.

“Nawapongeza wachezaji wangu kwa kazi kubwa waliyofanya sasa tunarejea nyumbani kwenda kujiandaa na mchezo wa mwisho dhidi ya Jwaneng,” amesema Benchikha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news