Simba SC yatoka sare tasa na ASEC Mimosas

ABIDJAN-Mchezo wa Simba SC wa hatua ya makundi ya Ligi Kuu ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas uliopigwa Uwanja wa Félix Houphouët-Boigny umemalizika kwa sare ya bila kufungana.
Mchezo ulianza kwa kasi ya kawaida huku timu zote zikishambuliana kwa zamu huku mpira ukichezwa zaidi katikati ya uwanja.

Kipindi cha pili Simba SC walirudi kwa kasi kwa kuliandama lango la ASEC ambapo dakika ya 46 Sadio Kanoute alipoteza nafasi ya wazi baada ya kumzidi ujanja mlinda mlango,lakini shuti lake lilitoka pembeni kidogo.

Waliendelea kutengeneza nafasi huku wenyeji ASEC nao wakija golini kwao mara kadhaa, lakini hakuna aliyeweza kutumia nafasi zilizopatikana.

Matokeo hayo yanaifanya Simba SC kuendelea kubaki nafasi ya pili wakiwa na alama sita baada ya kucheza mechi tano.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news