NEC yatoa vibali vya elimu ya mpiga kura na watazamaji wa uchaguzi mdogo wa udiwani kata 23

DODOMA-Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika kikao chake cha Februari 24, 2024, kilichofanyika katika Ofisi za Tume jijini Dodoma imetoa vibali vya kutoa elimu ya mpiga kura wakati wa uchaguzi mdogo wa Udiwani.

Ni katika kata 23 za Tanzania Bara utakaofanyika Machi 20, 2024 kwa asasi za kiraia 11.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima, R. K imeainisha asasi za kiraia 11 ambazo zimekidhi vigezo na kupewa vibali vya kutoa elimu ya mpiga kura.

Sambamba na kata walizoomba kutoa elimu hiyo kuwa ni Mbogwe Legal Aid Organization (MBOLAO) Isebya iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe, Sustainable Hub for Policy Initiatives (SHPI) Mshikamano iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Musoma.

Asasi zingine ni Promotion and Women Development Association (PWDA) Kasingirima iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji,

Bagamoyo Community Capacity Empowerment and Education (BCCEE) Fukayosi iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Action for Democratic Governance (A4DG) Kimbiji iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni.

Asasi zingine ni Vanessa Foundation ambayo itatoa elimu katika kata ya Nkokwa iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Tanzania Centre for Disability Development Initiatives (TCDDI) Nkokwa iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyela,

Safe Society Platform Tanzania (SSPT) Busegwe iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Butiama na Isebya iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe

Asasi zingine za kiraia zilizopata kibali ni Youth Against Aids and Poverty Association (YAAPA) ambayo itatoa elmu katika kata ya Kasingirima iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji, Musoma Municipal Paralegal Organisation (MMPO) Mshikamano iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Musoma.

Asasi nyingine iliyopata kibali ni Shirika la Elimu ya Uraia na Uzalendo “Civic Education and Patriotism Association” iliyoomba kutoa Elimu katika kata za Kimbiji iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni,

Msangani iliyopo katika Halmashauri ya Mji Kibaha, Fukayosi iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Mlanzi iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti na Kibata iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa.

Wakati huo huo, tume pia imetoa kibali kwa asasi za kiraia tatu ambazo zimekidhi vigezo ili ziweze kutazama uchaguzi mdogo wa Udiwani katika Kata 23 za Tanzania Bara.

Asasi hizo tatu zitakazoenda kutazama uchaguzi Mdogo wa udiwani siku ya Jumatano tarehe 20 Machi, 2024 ni Tanzania Alliance for Disability Development Initiatives itakayokuwa katika kata ya Mhande iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba,

Bridge Development Trust Organisation itakuwa katika kata ya Buzilasoga iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema na Promotion and Women Development Association itayokuwa katika Kata ya Kasingirima iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji.

Aidha, katika kikao hicho, Tume imezitaka asasi za kiraia zilizopata kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura, kuzingatia Mwongozo wa Elimu ya Mpiga Kura wa Mwaka 2020 katika kipindi chote cha kutoa elimu hiyo katika uchaguzi mdogo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news