NMB kuendelea kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu

DODOMA-Uongozi wa Benki ya NMB waahidi kuendelea kuunga mkono shughuli za Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu katika kuhakikisha wanaimarisha mahusiano yaliyopo na kuendelea kushirikiana katika utekelezaji wa majukumu yao ya kuratibu shughuli za Serikali.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akipokea zawadi kutoka uongozi wa Benki ya NMB, anayekabidhi ni Mkuu wa Idara ya Huduma za Kibenki kwa Serikali na Ofisi ya Makao Makuu Ndogo ya NMB- Dodoma, Bi. Vicky Bishubo walipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Idara ya Huduma za Kibenki kwa Serikali na Ofisi ya Makao Makuu Ndogo ya NMB- Dodoma, Bi Vicky Bishubo wakati walipotembelea na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Dkt. Jim Yonazi pamoja na Naibu wake Bw. Anderson Mutatebwa ofisini kwake Jijini Dodoma.

Alisema kuwa, katika kutoa huduma za kibenki ambazo zinahusu ofisi ya Waziri Mkuu wataendelea kuyafikia makundi mbalimbali ikiwemo vijana kwa kutoa huduma za kibenki popote walipo na hii itasaidia kusukuma juhudi za Serikali katika huduma za kifedha.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bw. Anderson Mutatembwa akipokea zawadi kutoka uongozi wa Benki ya NMB, anayekabidhi ni Mkuu wa Idara ya Huduma za Kibenki kwa Serikali na Ofisi ya Makao Makuu Ndogo ya NMB- Dodoma, Bi Vicky Bishubo walipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonazi akizungumza na baadhi ya viongozi wa Benki ya NMB walipomtembelea ofisini kwake Jijini Dodoma.

“Tumeendelea kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, na hii haitokuwa mwisho tunaahidi kuendelea kufanya hivyo katika kuunga mkono shughuli mnazotekeleza,” alisema Vicky.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi alisema kuwa, Benki ya NMB imefanya jambo muhimu kuitembelea ofisi yake na kueleza namna ilivyojipanga kuhakikisha inaunga mkono shughuli za Serikali na kuwasihi waendelee kufanya hivyo kadiri inavyofaa.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Bw. Anderson Mutatembwa akizungumza na baadhi ya viongozi wa Benki ya NMB walipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma.
Mkuu wa Idara ya Huduma za Kibenki kwa Serikali na Ofisi ya Makao Makuu Ndogo ya NMB Dodoma, Bi Vicky Bishubo akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bw. Anderson Mutatembwa walipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma. (Picha na OWM).

“Ninawapongeza NMB kwa moyo huu na mmetupa kuona umuhimu wa kuimarisha umoja uliopo nitoe wito muendelee kutoa huduma bora za kibenki kwa jamii yetu ili wananchi waendelee kunufaika na uwepo wenu na kujiletea maendeleo yao na Taifa kwa ujumla,” alisema Dkt. Yonazi.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Anderson Mutatebwa aliwashukuru NMB kwa kuitembelea ofisi hiyo na kuahidi kuendeleza ushirikiano uliopo bana yao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news