Rais Dkt.Mwinyi azidi kuwatafutia fursa wakulima wa mwani

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amemhakikishia Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. David Concar na ujumbe wake kuwa Serikali ya Zanzibar iko tayari kushirikiana na Nutri-Sun Limited kutoka Uingereza katika kukamilisha mradi wa kiwanda cha kuchakata mwani kilichopo Chamanangwe, Pemba ambacho kukamilika kwake kutawanufaisha kwa kurahisisha kupata soko la uhakika.
Katika salamu zake naye Balozi wa Uingereza nchini Mhe. David Concar amemweleza Rais Dk. Mwinyi kwamba mipango ya kupata mashine na teknolojia ya kuchakata mwani imekamilika hivyo ifikapo mwishoni mwa mwaka 2024 kiwanda hicho kitaanza kuzalisha Carrageenan ambayo itatatumika kwa matumizi ya viwanda vya chakula na matibabu.
Aidha, Bi. Marisa Drew kutoka Benki ya Standard Chartered alimhakikishia Rais Dkt. Mwinyi upatikanaji endelevu wa fedha ambazo zitatumika kununulia mashine na zao la mwani, kiwanda hicho kitawawezesha wakulima wa mwani hasa wanawake na vijana kujikwamua kiuchumi.

Rais Mheshimiwa Dkt.Mwinyi amekutana na ujumbe huo Februari 19,2024 Ikulu jijini Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news