Simba SC yazitaka alama tatu kutoka JKT Tanzania

DAR ES SALAAM-Kocha wa Makipa wa Klabu ya Simba, Daniel Cadena amesema, kikosi chake kipo kwenye hali nzuri kuelekea mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya JKT Tanzania utakaopigwa Uwanja wa Meja Jenerali Michael Isamuhyo saa 10 jioni.
Cadena amesema licha ya ratiba kuwa ngumu kutokana na kucheza mechi kila baada ya siku mbili wamejipanga vizuri kuhakikisha wanawapa furaha mashabiki kwa kupata alama tatu.

Kocha Cadena ameongeza kuwa, utakuwa mchezo mgumu hasa ukizingatia wapinzani wao hawapo kwenye nafasi nzuri, lakini wapo tayari kuwakabili.

“Tunajivunia kuwa na wachezaji bora ambao wanacheza kila baada ya muda, lakini wanapambana na kuhakikisha tunapata ushindi.”

“Nategemea kuwaona mashabiki wetu wengi uwanjani na tunajua wanahitaji furaha nasi tutajitahidi kuhakikisha tunawapatia,” amesema Kocha Cadena.

Naye nahodha, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesema, wachezaji wote wapo timamu kimwili na kiakili kuhakikisha wanapambana ili pointi tatu zipatikane.

“Haitakuwa mechi rahisi, tunawajua JKT ni timu nzuri lakini tumejipanga na tutaingia kwenye mchezo kwa lengo la kutafuta pointi tatu,” amesema Zimbwe Jr.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news