Thadei Ole Mushi afariki

DAR ES SALAAM-Mchambuzi mahiri na mtetezi kabambe wa siasa za Chama Cha Mapinduzi (CCM), Thadei Ole Mushi amefariki.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa katika ukurasa wa Facebook na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka.
"Kaka rafiki na ndugu yangu Thadei Ole Mushi -Mungu Baba yetu Akupe Pumziko la Milele Mbinguni, Kizazi Chetu kimepoteza Mwalimu,Mchambuzi na Mwanajamii KIJANA aliyetumia maarifa na kalamu yake kutoa maoni na hisia zake katika nyanja nyingi za Kijamii,Kisiasa,kiuchumi nk.

"Maandishi yako yataishi,Hakika umetuliza sisi marafiki zako,Mimi na Familiya yangu-Tunatoa pole nyingi sana kwa familiya yako,mke na wanao,wazazi na ndugu zako.Hakika Hii Dunia Tuu wapitaji-Tuonane kwenye Ile asubuhi njema na Iliyo Kuu. Nimekuwa Speechless #MachoziYangu,"amefafanua Mtaka.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news