Ubalozi wa Marekani kufanya mnada wa mali mbalimbali Dar

DAR ES SALAAM-Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam unapenda kutangaza kuwa utauza mali mbalimbali katika mnada utakaofanyika tarehe 10 Februari 2024, kuanzia saa 3 asubuhi.
Mnada huu utaendeshwa na kufanyika UNIVERSAL AUCTION CENTRE, iliyoko karibu na Golden Resort, Lion Street, Sinza, Dar es Salaam (Angalia ramani).

Vitu vyote vitauzwa "kama vilivyo" bila garantii, huku kodi zote na ushuru ukiwa jukumu la mnunuzi. Maegesho ya magari ni machache.

Ni watu 200 tu wa mwanzo ndio watakaoruhusiwa kuingia katika mnada, hivyo tunapendekeza ufike mapema.

Unaweza kutazama vitu vitakavyouzwa siku ya Alhamisi, tarehe 8 Februari, na Ijumaa, tarehe 9 Februari kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 11 jioni.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news