UVCCM wamshukuru Prof.Muhongo

NA FRESHA KINASA

VIONGOZI na wanachama wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)Wilaya ya Musoma Vijijini wamemshukuru Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo kwa jinsi anavyofuatilia fedha kutoka serikalini ambazo zimekuwa zikifanikisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Wameyasema hayo Februari 3, 2024 wakati wakiongea na DIRAMAKINI wakati wa sherehe za miaka 47 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi yaliyofanyika kijijini Kakisheri Kata ya Nyakatende ambapo Mbunge Prof. Muhongo ameendelea kuchangia kufanikisha sherehe hizo.

"Tunamshukuru Prof. Muhongo fedha nyingi kutoka serikalini zimeletwa jimboni mwetu kujenga miradi ya maji, miradi ya barabara, miradi ya afya fedha hizi zimeletwa kutokana na ufuatiliaji wake madhubuti lakini pia Rais Dkt. Samia tumshukuru kwa kutoa fedha hizo na Jimbo letu limeendelea kupiga hàtua," amesema Jumanne Bwire mwanachama wa UVCCM jimboni humo.

"Tunaoana Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma imejengwa na sasa inatoa huduma kwa wananchi huu ni uongozi mzuri wa Dkt. Samia Hassan na Mbunge wetu kuona tunapata huduma za afya karibu.

"Na pia Mbunge amekuwa na kampeni ya ujenzi wa maabara katika shule za sekondari jimboni mwetu lengo ni kuandaa wana sayansi bora wa siku za usoni," amesema Nyafuru Bwire Mussa mwanachama UVCCM Nyakatende.

"Mbunge amekuwa wazi kwa fedha za Mfuko wa Jimbo, na pia fedha hizo zimekuwa zikinufaisha wananchi kwa kugharamia miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa yeye ni mpenda maendeleo.

"Pia amekuwa akisimama na wananchi katika majanga mbalimbali yanapotokea tunamshukuru sana kwa uwajibikaji wake na kutujali wananchi,"amesema Mathias Maira mwanachama UVCCM.

Shabani Mafuru ameiambia DIRAMAKINI kuwa anaishukuru Serikali, viongozi wa CCM jimboni humo pamoja na Mbunge Prof. Muhongo kwa jinsi ambavyo utatuzi wa changamoto mbalimbali za maendeleo wamekuwa wakizitatua kwa pamoja kupitia mikutano ya hadhara kwa maendeleo ya wananchi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini imeeleza kuwa, "Jumuiya zote za CCM jimboni humo zimekamilisha sherehe zake.

"Chama kinaendelea kusherehekea kwenye ngazi za Kata. Na Mbunge waJimbo, Prof Sospeter Muhongo anachangia ufanikishaji wa sherehe hizi,"imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news