Fei Toto awapokonya Yanga SC alama tatu kupitia bao la dakika ya 51

DAR ES SALAAM-Aliyewahi kuwa kiungo wa Yanga SC,Feisal Salum 'Fei Toto' ametokea nyuma na kuwapokonya waajiri hao wa zamani alama tatu.
Ni kupitia bao la dakika 51 ambalo limeiwezesha Azam FC kushinda mabao 2-1 dhidi ya mabingwa watetezi, Yanga SC.

Mtanange huo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara umepigwa leo Machi 17,2024 Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Awali, Clement Francis Mzize alianza kuifungia Yanga dakika ya 10 huku Gibrill Sillah wa Azam FC dakika ya 19 akisawazisha.

Vile vile,Azam FC inafikisha alama 47 katika mchezo wa 21 ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa alama tano na Yanga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news