Prof.Muhongo azidi kufanya zaidi ya matarajio Musoma Vijijini

MARA-Jimbo la Musoma Vijijini linaloongozwa na Mbunge Mheshimiwa Prof. Sospeter Muhongo limebainisha utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika sekta ya elimu kwa kipindi cha 2020 hadi 2025 unavyoendelea.
Huku kukiwa na mageuzi makubwa ya kimaendeleo katika sekta hiyo.

Hatua hiyo inatokana na ushirikiano mzuri baina ya Wananchi jimboni humo na Mbunge wao Prof. Sospeter Muhongo pamoja na Serikali ya Awamu ya Sita katika kuimarisha sekta ya elimu jimboni humo kwa ufanisi mkubwa sana.

Prof. Muhongo amekuwa akiendelea na mikakati mbalimbali ya kuimarisha Sekta ya elimu akishirikisha wadau mbalimbali jimboni humo ili kulifanya Jimbo la Musoma Vijijini liwe na wasomi wengi mahiri wenye ujuzi katika kuchangia maendeleo ya nyanja mbalimbali hapa nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news