Serikali yadhamira kufikia maendeleo endelevu

NA FARIDA RAMADHANI
WF

WAZIRI wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amesema kuwa Serikali inaendelea kufanya jitihada mbalimbali kuhakikisha nchi inakuwa na maendeleo endelevu.
Meza kuu ikiongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (wa pili kushoto), Waziri wa Kazi, Uchumi na Uwekezaji - Zanzibar, Mhe. Shariff Ali Shariff (Mb) (wa kwanza kushoto), Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwenyekiti wa Kundi la Washirika wa Maendeleo nchini, Mhe. Zlatan Milišić (wa kwanza kulia) na Balozi wa Uingereza nchini ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Wadau wa Maendeleo, Mhe. David Concar (wa pili kulia), wakifuatilia kwa umakini Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakati wa Ngazi ya Juu 2024, wenye kaulimbiu,”Kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050; Kuongeza Kasi ya Uchumi Himilivu na Maendeleo Jumuishi katika Nyakati Zisizotabirika, uliohusisha Serikali, Washirika wa Maendeleo, Sekta Binafsi na Asasi Zisizo za Kiserikali, uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam.

Dkt. Nchemba alisema hayo jijini Dar es Salaam wakati akifungua Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakati kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo ngazi ya Juu.

Alisema kuwa Serikali chini ya uongozi wa Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, imedhamiria kuwa na maendeleo endelevu ambayo hayamuachi Mtanzania yoyote nyuma kwa kufanya uwekezaji katika Sekta za Uzalishaji.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (Kushoto), akiteta jambo na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwenyekiti wa Kundi la Washirika wa Maendeleo nchini, Mhe. Zlatan Milišić, wakati wa Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakati wa Ngazi ya Juu 2024, wenye kaulimbiu,”Kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050; Kuongeza Kasi ya Uchumi Himilivu na Maendeleo Jumuishi katika Nyakati Zisizotabirika, uliohusisha Serikali, Washirika wa Maendeleo, Sekta Binafsi na Asasi Zisizo za Kiserikali, uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania-BoT, jijini Dar es Salaam.

“Kipaumbele kimewekwa kwenye uwekezaji katika mtaji wa binadamu, maendeleo ya miundombinu, kuhamasisha ukuaji wa kiuchumi, kuimarisha utoaji wa huduma za kijamii, utawala bora, kuwawezesha wanawake na uhifadhi wa mazingira”, alibainisha Mhe. Nchemba.

Alisema kuwa kwa kutekeleza mikakati hiyo pamoja na kukuza ushirikiano na sekta binafsi, asasi za kiraia na washirika wa maendeleo, Tanzania inaweza kupiga hatua kubwa kuelekea kufikia ukuaji wa Uchumi endelevu.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akihutubia wakati wa Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakati wa Ngazi ya Juu 2024, wenye kaulimbiu,”Kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050; Kuongeza Kasi ya Uchumi Himilivu na Maendeleo Jumuishi katika Nyakati Zisizotabirika, uliohusisha Serikali, Washirika wa Maendeleo, Sekta Binafsi na Asasi Zisizo za Kiserikali, katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam.

Dkt. Nchemba alisema Serikali inatambua umuhimu wa kuimarisha mazingira ya ukuaji wa biashara, kuongeza ushindani na kukuza ubunifu ili kukuza uchumi wa nchi.

Aidha, Dkt. Nchemba, alisema Tanzania pia inatumia Diplomasia ya Kiuchumi kama mkakati muhimu wa kuendeleza uchumi wake na kubainisha kuwa nchi ina dhamira kubwa ya kufuata kanuni za ushirikiano wa kimataifa wenye manufaa kwa pande zote.
Mwenyekiti Mwenza wa Kundi la Washirika wa Maendeleo, Mhe. Balozi David Concar, ambaye pia ni Balozi wa Uingereza nchini, akizungumza wakati wa Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakati wa Ngazi ya Juu 2024, wenye kaulimbiu,”Kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050; Kuongeza Kasi ya Uchumi Himilivu na Maendeleo Jumuishi katika Nyakati Zisizotabirika, uliohusisha Serikali, Washirika wa Maendeleo, Sekta Binafsi na Asasi Zisizo za Kiserikali, uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania-BoT, jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake, Balozi wa Uingereza nchini Tanzania na Mwenyekiti Mwenza wa Mkutano huo, Mhe. David Concar, alisema kuwa wadau wa maendeleo wanampongeza Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoyafanya na wanayaona mabadiliko mbalimbali anayofanya katika kuboresha mazingira ya uwekezaji, biashara pamoja na uwekezaji katika sekta ya uzalishaji.

Alisema kuwa wadau wa maendeleo wako tayari kuendelea kuiwezesha nchi kufikia maendeleo ya kukuza uchumi wa wananchi.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (wa pili kushoto walioketi), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji - Zanzibar, Mhe. Shariff Ali Shariff (Mb) (kushoto), Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwenyekiti wa Kundi la Washirika wa Maendeleo nchini, Mhe. Zlatan Milišić (wa kwanza kulia walioketi) na Balozi wa Uingereza nchini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Washirika wa Maendeleo, Mhe. David Concar (wa pili kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakati wa Ngazi ya Juu 2024, wenye kaulimbiu,”Kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050; Kuongeza Kasi ya Uchumi Himilivu na Maendeleo Jumuishi katika Nyakati Zisizotabirika, uliohusisha Serikali, Washirika wa Maendeleo, Sekta Binafsi na Asasi Zisizo za Kiserikali, uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania-BoT, jijini Dar es Salaam.

Mhe. Concar alisema wadau wa maendeleo wametoa zaidi ya Dola bilioni 2.7 kwa ajili ya kuisaidia Tanzania kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo asilimia 51 ya fedha hizo ni misaada na asilimia 49 ni mikopo yenye masharti nafuu.
Washirika mbalimbali wa Maendeleo nchini wakifuatilia kwa umakini Hotuba ya Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (hayupo pichani), wakati akifungua Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakati wa Ngazi ya Juu 2024, wenye kaulimbiu,”Kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050; Kuongeza Kasi ya Uchumi Himilivu na Maendeleo Jumuishi katika Nyakati Zisizotabirika, uliohusisha Serikali, Washirika wa Maendeleo, Sekta Binafsi na Asasi Zisizo za Kiserikali, uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania-BoT, jijini Dar es Salaam.
Alibainisha kuwa, asilimia 40 ya fedha hizo zilitolewa na nchi moja moja za washirika wa maendeleo na asilimia 60 za fedha hizo zimetolewa na Taasisi za Kimataifa za fedha ikiwemo Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).

Nao washiriki wa mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa SRF, Prof. Fortunata Makene na Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA, Dkt. Donald Mmari, walisema kuwa majadiliano hayo ni muhimu kwa maendelo ya nchi kwa kuwa yanaikutanisha Serikali na wadau wa maendeleo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news