TIC yasajili miradi 1,188 miaka mitatu ya Rais Dkt.Samia

NA GODFREY NNKO

KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesajili jumla ya miradi 1,188 ambayo ilikadiriwa kuwekeza kiasi cha mtaji wa dola za Marekani milioni 15,041 na kutoa jumla ya ajira 345,464.Hayo yamesemwa leo Machi 24, 2024 jijini Dar es Salaam na Msemaji Mkuu wa Serikali,Mobhare Matinyi wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya miaka mitatu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan madarani.

Akieleza kuhusu suala la uwekezaji katika kipindi kuanzi Machi, 2021 hadi Machi,2024 amesema, kati ya miradi hiyo asilimia 35 inamilikiwa na Watanzania.

Vile vile asilimia 41 ya miradi ni ya wageni na asilimia 24 ni ya ubia kati ya Watanzania na wageni nchini.

Pia, amesema kuwa Kamati ya Kitaifa ya Kusimamia Uwekezaji (National Investment Steering Committee– NISC) ilitoa idhini ya kusainiwa mikataba ya utekelezaji kwa miradi 16.

“Miradi hiyo yenye hadhi ya miradi mahiri ni pamoja na Mradi wa Bagamoyo Sugar Limited,Mradi wa Kagera Sugar Limited na Mradi wa Mtibwa Sugar Estate Limited."

Amesema, NISC iliridhia miradi mingine nane ambayo ilisaini mikataba ya utekelezaji na TIC baada ya kupewa hadhi ya kuwa wawekezaji mahiri maalum.

“Katika kundi hili kuna wa upanuzi wa kiwanda cha kuzalisha sukari wa Kampuni ya Kilombero Sugar Limited na pia mradi wa kilimo cha miwa na kiwanda cha kuzalisha sukari wa Kampuni ya Mufindi Paper Mills Limited- Kasulu,”amesema Matinyi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news