Waziri Mkuu aacha shangwe Musoma Vijijini

NA FRESHA KINASA

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa amewaeleza wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini kuhusu uamuzi wa Serikali kuendelea kutoa fedha nyingi za utekelezaji wa miradi ya maendeleo jimboni humo.
Amesema, Serikali ya Dkt.Samia Suluhu Hassan imejidhatiti kikamilifu kuona Jimbo la Musoma Vijijini linaloongozwa na Mbunge Prof. Sospeter Muhongo linakuwa na miradi ya maendeleo ambayo inagusa maisha ya wananchi moja kwa moja katika sekta ya barabara, maji, elimu na afya.

Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassimu Majaliwa aliyasema hayo kwenye mkutano wake wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Bwai Kwitururu, Musoma Vijijini siku ya Alhamisi ya Februari 29,2024 wakati akiwa katika siku ya tano ya ziara yake mkoani humo iliyoanza kuanzia Februari 25, 2024 hadi Februari 29, 2024.
Mheshimiwa Majaliwa amewataka wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini kuendelea kuiamini Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Dkt. Samia Hassan na pia aliwaomba kuendelea kumuamini Mbunge wao Prof. Sospeter Muhongo kwani ni kiongozi mahiri na mwenye heshima kubwa serikalini hivyo ni kiongozi anayefaa kuzidi kuwaletea maendeleo.

Katika mkutano huo, Mawaziri wa Wizara mbalimbali pia walipata fursa ya kuelezea jinsi ambayo miradi mbalimbali ya Wizara wanazozisimamia itakavyotekelezezwa kwa Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini.

Godfrey Kasekenya ni Naibu Waziri wa Ujenzi akizungumza katika mkutano huo alisema, Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kujenga barabara kuu la Musoma-Makojo-Busekera yenye urefu wa kilometa 92 kwa kiwango cha lami.

Ambapo, kilomita tanl zimeishawekewa lami, na barabara hiyo ipo kwenye Bajeti ya mwaka huu (2023/2024) huku akisema kuwa kibali kimetolewa barabara itangazwe na Mkandarasi apatikane, na aendelee na ujenzi.

Kwa upande wao wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini wanaendelea kuishukuru Serikali chini ya uongozi mzuri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha nyingi za kufadhili miradi ya maendeleo.

"Tunamshukuru sana Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa kwa kututembelea Jimboni mwetu, na kwa kuendelea kufuatilia utekelezaji wa miradi yetu ya maendeleo ambayo ni kielelezo cha mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2020-2025,"imeeleza sehemu ya taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa jimbo hilo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news