Wizara ya Mambo ya Nje kushiriki Maonesho Maalum kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani

DODOMA-Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inashiriki maonesho maalum ya wanawake yanayofanyika kimkoa katika viwanja vya Mashujaa jijini Dodoma kuanzia tarehe 07 hadi 11 Machi 2024 ikiwa ni maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani itakayofanyika duniani kote tarehe 08 Machi 2024.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Kawina Kawina akimsikiliza Afisa Mambo ya Nje, Bi. Elizabeth Bukwimba akimweleza kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya ushiriki wa Wizara kwenye maonesho maalum yatakayofanyika katika Viwanja vya Mashujaa jijini Dodoma kuanzia tarehe 07 hadi 11 Machi 2024 ikiwa ni maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani itakayoadhimishwa duniani kote tarehe 08 Machi 2024. Bw. Kawina ametembelea banda hilo tarehe 06 Machi 2024 kukagua hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya ushiriki wa wizara.

Maonesho hayo ambayo yanaratibiwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma yatafunguliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Rosemary Senyamule tarehe 07 Machi 2024.

Huduma zitakazotolewa katika Banda la Wizara wakati wa maonesho hayo ni pamoja na uthibitishaji wa nyaraka mbalimbali ikiwemo vyeti vya taaluma, ndoa na nyaraka nyingine, zoezi ambalo litaanza rasmi tarehe 07 hadi 11 Machi, 2024.
Bw. Kawina akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Wizara kukagua maandalizi ya ushiriki wa Wizara katika maonesho maalum kuelekea siku ya wanawake duniani yanayofanyika katika viwanja vya mashujaa jijini Dodoma kuanzia tarehe 07 hadi 11 Machi 2024. Wanaoshuhudia ni Watumishi kutoka Taasisi za Wizara akiwemo Badriya Masoud (kulia), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa APRM, Bi. Praxeda Gaspar kutoka APRM na Bi. Susan Masawe kutoka Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim.

Taarifa nyingine ni kuhusu utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje na mchango wa wanawake kwenye medani za kimataifa na diplomasia.

Kadhalika maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Taasisi zilizo chini ya Wizara ambazo ni Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim zamani Chuo cha Diplomasia; Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC) na Mpango wa Hiari wa Kujipima kwa Vigezo vya Utawala Bora (APRM) yatatolewa.
Bw. Kawina akikagua vipeperushi vitakavyogawiwa kwa wananchi watakaotembelea banda la Wizara wakati wa maonesho maalum kuelekea siku ya wanawake duniani yanayofanyika jijini Dodoma katika viwanja vya mashujaa kuanzia tarehe 07 hadi 11 Machi 2024.
Afisa kutoka Taasisi ya Wizara ya Mpango wa Hiari wa Kujipima kwa Vigezo vya Utawala Bora (APRM), Bi. Praxeda Gaspar akimpatia Bw. Kawina kipeperushi kuhusu taasisi hiyo.
Bw. Kawina akipata maelezo kutoka kwa Bi. Janeth Benedict kutoka Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC) kuhusu vipeperushi watakavyosambaza kwa wananchi kuhusu taasisi hiyo.
Muonekano wa banda la wizara.

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa mwaka 2024 yamebeba kaulimbiu isemayo "Wekeza kwa Wanawake kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii".

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news