DCEA yaendelea kutoa elimu kuhusu dawa za kulevya katika Maadhimisho ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahala Pa Kazi jijini Arusha

ARUSHA-Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini imetoa elimu kinga dhidi ya tatizo la dawa za kulevya katika Maadhimisho ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahala Pa Kazi yanayofanyika katika viwanja vya General Tyre vilivyopo Njiro jijini Arusha.

Maadhimisho hayo yameanza Aprili 23,2024 na yatamalizika Aprili 30,2024 yakiongozwa na kauli mbinu ya mwaka huu ya "Athari ya Mabadiliko ya Tabia ya Nchi katika Usalama na Afya Kazini".
Pamoja na kutoa elimu ya dawa za kulevya kwa ujumla, maafisa wanazungumzia pia uhusiano mkubwa uliopo kati ya tatizo la dawa za kulevya na usalama na afya mahala pa kazi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news