Katibu Mkuu Kiongozi atoa wito kwa Mabalozi wa Tanzania duniani

PWANI-Mabalozi wamehimizwa kutumia taaluma, uzoefu na ujuzi tofauti waliokuwa nao kuharakisha mabadiliko ya kimfumo yanayoendelea ndani ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Kauli hiyo imetolewa leo Aprili, 23, 2024 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka wakati anaongea na Mabalozi katika warsha ya siku nne ya kutathimini utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje inayofanyika mjini Kibaha mkoani Pwani tokea tarehe 21 Aprili 2024.
"Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki mmebarikiwa kuwa na watu wenye taaluma tofauti na wenye historia ya sekta tofauti, tumieni fursa yenu hii kumsadia Mwanadiplomasia namba moja, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amewarahisishia kazi yenu kwa kuitekeleza diplomasia kivitendo," Balozi Kusiluka amesisitiza.
Amesema, Serikali inazitambua changamoto wanazokabiliana nazo na inazifanyia kazi lakini kutokana na Wizara kuwa na watu wenye uzoefu wa kutoka sekta tofauti, wakishirikiana wanaweza kuzitatua na kuifikisha nchi katika hatua nzuri.
Balozi Kusiluka alimazia kwa kuwapongeza Mabalozi kwa kazi nzuri wanayofanya na kuwaahidi kuwa Serikali itapokea mawazo yote mazuri na ya kibunifu na kuyafanyia kazi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news