RC Chalamila asema Dar ipo salama, TANROADS na TARURA wapo kazini

DAR ES SALAAM-Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Albert Chalamila leo Aprili 23, 2024 ametembelea na kukagua maeneo yaliyoathirika na mvua katika Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Akiwa katika ziara hiyo RC Chalamila amekagua miundombinu mbalimbali ikiwemo daraja la Kibada ambapo TANROADS wanaendelea na matengenezo ya daraja hilo ili kurejesha mawasiliano.

Aidha,RC Chalamila amewatoa hofu wananchi kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha ambapo amesema Dar Es Salaam ni salama hakuna barabara ambayo itaachwa bila kutengenezwa barabara zote zitatengenezwa katika viwango tofauti "wananchi waendelee kuchukua tahadhari ikiwemo kuhama mabondeni,"amesema RC Chalamila.
Vilevile,Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa ameelekeza kuanza kwa operesheni ya kuondoa vipenyo ili kuruhusu maji yapite ikiwemo kubomoa kuta zinazozuia maji kupita.

Sambamba na hilo RC Chalamila amezitaka halmashauri zote katika mkoa huo kutoa fedha ambazo ziliwekwa katika bajeti kwa ajili ya TARURA ili kuharakisha urekebishaji wa maeneo yote yaliyoharibiwa na mvua.
Mwisho RC Chalamila amezitaka TANROADS na TARURA kufanya kazi usiku na mchana katika nyakati hizi za mvua "Kabla ya usiku wa kesho Aprili 24, 2024 barabara ziwe zinapitika."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news