Kila anayefika Banda la PSSSF Maonesho ya OSHA jijini Arusha anatabasamu kwa huduma bora

ARUSHA-Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) ni miongoni mwa taasisi na mashirika ya umma ambayo yanashiriki katika Maadhimisho ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahala Pa Kazi yanayofanyika katika viwanja vya General Tyre vilivyopo Njiro jijini Arusha.

Kupitia maadhimisho hayo ambayo yameanza Aprili 23,2024 huku yakitarajiwa kufikia tamati Aprili 30,2024 watumishi wa PSSSF wamekuwa mstari wa mbele kutoa elimu na huduma kwa wanachama mbalimbali. 

Na kila anayeingia katika banda hilo amekuwa akitoka na tabasamu kutokana na huduma bora anayopata.
Meneja wa PSSSF Kanda ya Kaskazini,Bi. Vonness Koka (kushoto) akitoa elimu ya kutumia huduma ya PSSSF Kiganjani kwa Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika maonesho ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) yanayoendelea katika viwanja vya General Tyre, Njiro jijini Arusha leo Aprili 24,2024.
Mmoja wa Wanachama wa PSSSF akionesha simu yake ya mkononi baada ya kupakua application ya PSSSF Kiganjani alipotembelea Banda la PSSSF Katika maonesho ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) yanayoendelea katika viwanja vya General Tyre Njiro, jijini Arusha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news