Rais Dkt.Mwinyi afungua Mkutano wa SADCOPAC

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali zote mbili, ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Mapinduzi ya Zanzibar zinafanya jitihada kubwa kukabiliana na vitendo vya rushwa na kuhimiza uwajibikaji ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 pamoja na mipango mingine ya maendeleo.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo leo Aprili 17,2024 alipofungua rasmi Mkutano wa mafunzo kwa wajumbe na wataalam wa kamati ya SADCOPAC katika kupambana na rushwa , kuhamasisha uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa maliasili unaofanyika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, uwanja wa ndege Zanzibar.
Aidha,Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa Zanzibar inasimamia masharti na maelekezo ya miongozo ya kamati ya SADCOPAC kwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha inatekeleza kikamilifu makubaliano yaliyoafikiwa baina ya nchi wanachama.
Rais Dkt.Mwinyi amesema Zanzibar imeanzisha utaratibu wa kusomwa hadharani taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na kujadiliwa kwa uwazi na kina katika Baraza la Wawakilishi.
Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi ametoa wito kwa nchi wanachama wa SADC kuziimarisha taasisi zinazohusika na utawala bora kwa kuzipatia wataalam zaidi wa fani mbalimbali ili ziwe na upeo mkubwa zaidi wa kufanya uchunguzi kwa mujibu wa majukumu yao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news